Jumanne, tarehe 12 Agosti 2025, Chuo cha SomaIT kiliendesha semina ya mafunzo kwa wafanyakazi wa Bodi ya Huduma za Maktaba Zanzibar.
Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo katika matumizi ya Artificial Intelligence (Akili Bandia) ili kuboresha huduma na ufanisi wa kazi za maktaba.
Chuo cha SomaIT kiliwakilishwa na Mkuu wa Chuo, Khalifa Saidi Khamisi, Mratibu wa Chuo, Ahmed Rashid, pamoja na Mhadhiri, Ramadhan Yasin.
Mapokezi kutoka kwa Uongozi wa Bodi ya Huduma za Maktaba Zanzibar yalikuwa ya kipekee, na Chuo cha SomaIT kinatoa shukrani za dhati kwa ushirikiano uliotolewa.
Ni matumaini ya chuo kuwa mafunzo haya yatakuwa chachu ya ubunifu na maendeleo katika sekta ya huduma za maktaba Zanzibar.