Tarehe 19 Juni 2025 tumeshuhudia hatua muhimu ya maendeleo.
Tumefanikisha kusaini Makubaliano ya Ushirikiano (MOU) kati ya Somait Institute of Technology na Karibu Net, yakisainiwa rasmi na Mkuu Msaidizi wa Chuo, Bw. Yusuf Hassan, na Mkurugenzi wa Karibu Net, Bw. Abdul Hamid Hassan.
Lengo kuu la makubaliano haya ni kuchochea maendeleo ya teknolojia kwa vijana na jamii nzima ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.